• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, FIFA yaonya kuzifungia Ghana na Nigeria

    (GMT+08:00) 2018-08-15 11:13:58

    Shirikisho la soka duniani FIFA limeonya kuzifungia uanachama nchi za Nigeria na Ghana endapo hazitatekeleza matakwa ya kanuni zinazoongoza shirikisho hilo.

    Nigeria wameingia matatani baada ya serikali kutoa amri ya kufutwa kwa matokeo na kuamuru uchaguzi mkuu wa Rais wa Shirikisho la Soka la Nigeria NFF urudiwe ikiwa ni baada ya mgombea aliyeshindwa kwenda mahakama za kiraia kukata rufaa, jambo ambalo ni kinyume na kanuni za FIFA za kutotaka mambo yake kuingiliwa.

    Katika uchaguzi huo Rais wa sasa NFF Amanju Pinnick alimshinda mgombea mwenzake Chris Giwa, na kutokana na rufaa aliyokata serikali inataka Pinnick asitambuliwe kwa madai kuwa hakushinda kihalali.

    Nchini Ghana mahakama ilitoa hukumu inayoitaka serikali kulifuta Shirikisho la soka la nchi hiyo GFA kutokana na kashfa za rushwa kubwa kubwa zilizopelekea kusimamishwa kwa Rais wa GFA Kwesi Nyantaki, na FIFA ikitaka uamuzi huo usichukuliwe na endapo serikali itashikilia msimamo huo hadi Agosti 27 mwaka huu basi Ghana itafutiwa uanachama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako