• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Ulaya Leo: Atletico Madrid na Real Madrid kushindania kombe la UEFA Super Cup leo

    (GMT+08:00) 2018-08-15 11:14:19

    Mahasimu wa kihitsoria katika soka la Hispania, timu za Atletico Madrid na Real Madrid usiku wa leo zinakutana kwenye mechi ya kumtafuta bingwa wa jumla kisoka barani ulaya kwa msimu uliopita (UEFA Super Cup) itakayopigwa mjini Talinn nchini Estonia.

    Mechi hii itakuwa ya kwanza ya kiushindani kwa kocha mpya wa Real Julien Lopetegui tangu aanze kuifundisha, changamoto ikiwa ni dunia kuwa kiu kubwa ya kuona ufanisi wa timu hiyo bila Cristiano Ronaldo kwa kipindi kifupi tangu alipoondoka.

    Kwa upande wao Atletico ambao katika misimu ya hivi karibuni wamekuwa mwiba mkali kwa Real, watahitaji kuthibitisha ubora wakiwa na idadi kubwa ya wachezaji wazoefu na waliyoipa mafanikio timu hiyo chini ya kocha Diego Simeoni.

    Real Madrid ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo, wakiwa wameshinda mfululizo katika misimu miwili iliyopita na endapo watashinda mechi ya leo, ni basi kuwa wataandika rekodi mpya ya kutwaa mara tatu mfululizo, na wataingia rekodi ya kutwaa kombe hilo mara tano wakiungana na Barcelona pamoja na AC Milan ambazo pia zimewahi kushinda mara tano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako