• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Benki ya AfDB atoa wito wakulima wapewe teknolojia mpya

    (GMT+08:00) 2018-08-15 19:54:55
    Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ,Akinwumi Adesina ametoa wito wakulima barani Afrika wapewe teknolojia mpya zenye uwezo wa kuleta mageuzi katika kilimo.

    Adesina alisema ubadilishanaji wa teknolojia unahitajika na kwamba ushahidi kutoka nchi kama vile Nigeria umeonyesha kuwa teknolojia pamoja na kujitolea kwa serikali tayari kumeanza kuzaa matunda.

    Adesina aliyasema haya jana wakati akizungumza katika Mkutano wa mwaka wa Chama cha Kilimo na Sayansi ulioandaliwa jijini Washington D.C.

    Adesiana alisema Nigeria,ambako sera wakati wa utawala wake kama Waziri wa Kilimo,zilichangia katika mabadiliko ya uzalishaji wa mchele katika kipindi cha miaka mitatu.

    Adesina alisisitiza kuhusu azma ya Benki ya AfDB ya kubadilisha sura ya kilimo barani Afrika ili kufungua vyanzo vyenginevyo vya utajiri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako