Naibu Waziri wa Kilimo,utoshelevu wa chakula na vyama vya ushirika,Omar Mgumba amesema wizara yake inaelewa kuwa wakulima wa miwa wameshindwa kuuza bidhaa hiyo kwa kiwanda cha sukari cha Kilombero kwa sababu barabara na madaraja hayapitiki.
Alisema uboreshwaji wa miundombinu pia utasaidia kiwanda hicho kusafirisha sukari sokoni kwa urahisi haswa maeneo ya mijini.
Alisema serikali inajitahidi kuhakikisha kuwa inaboresha miundombinu katika wilaya ya Kilombero na mkoa wa Morogoro ili wakulima waweze kuuza miwa katika kiwanda cha Kilombero wakati wowote.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |