• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa Wakfu wa Tony Emelu kufanyika 25 Oktoba Lagos,Nigeria

    (GMT+08:00) 2018-08-16 20:14:24
    Takriban wajasiriamali 5,000 kutoka barani Afrika wanatarajiwa kukongamana jijini Lagos,Nigeria mwezi Oktoba kwa ajili ya makala ya nne ya mkutano wa ujasiriamali wa Wakfu wa Tony Emelu,TEF,unaosemekana kuwa mkutano mkubwa zaidi wa ujasiriamali.

    WQakfu wa Tony Emelu umetangaza tarehe 25 Oktoba kuwa tarehe ya mkutano huo wa ujasiriamali,unaotarajiwa kuvutia maelfu ya wajasiriamali wanaochipuka kutoka sehemu mbalimbali za Afrika,wengi wao wakiwa ni walionufaika na wakfu huo.

    Wakfu wa Tony Emelu,ambao unatoa msaada wa ujasiriamali wa $100 milioni unalenga kuwawezesha wajasiriamali 10,000 waafrika katika kipindi cha miaka 10.

    Kila mwaka wakfu huo huchagua wajasiriamali 1,000 kutoka sehemu mbalimbali za Afrika kupata mafunzo ya wiki 12,ushauri,na kuwapa mtaji wa $10,000 .

    Mkutano huo wa TEF huwa ndio mwisho wa ratiba ya kila mwaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako