• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapenda kunufaika kwa pamoja na nchi mbalimbali duniani kwenye viwanda vya roboti

    (GMT+08:00) 2018-08-17 14:24:08

    Waziri wa viwanda na upashanaji wa habari wa China Bw. Miao Wei amesema, China ina mahitaji makubwa ya roboti. Katika mchakato wa kuhimiza maendeleo yenye kiwango cha juu cha viwanda vya roboti, China itashikilia wazo la kufungua mlango, na itajenga utaratibu wa roboti ulio wazi na ushirikiano ili kunufaisha pande zote.

    Mkutano wa roboti wa dunia kwa mwaka 2018 unaofanyika mjini Beijing umeshirikisha kampuni zaidi ya 160 za roboti duniani. Waziri wa viwanda na upashanaji wa habari wa China Bw. Miao Wei akihutubia ufunguzi wa mkutano huo anasema, katika miaka mitano iliyopita, thamani ya viwanda vya roboti nchini China imekaribia asilimia 30 kwa mwaka, na kufikia dola bilioni 7 za kimarekani mwaka 2017, na uzalishaji wa roboti zinazotumiwa kwenye viwanda ulizidi laki 1.3, ambalo ni ongezeko la asilimia 68.1, na mwelekeo wa ongezeko la kasi kwenye viwanda hivyo utadumishwa. Bw. Miao Wei anasema:

    "China inaweka mkazo mkubwa katika kuendeleza viwanda vya roboti, na kuziweka hatua za kusukuma mbele teknolojia ya roboti na maendeleo ya sekta hiyo kuwa hatua muhimu ya kutekeleza mpango wa kimkakati wa kuijenga China iwe nchi yenye uwezo mkubwa wa kufanya matengenezo."

    Kwenye hotuba hiyo Bw. Miao Wei pia ameeleza bayana kuwa, hivi sasa viwanda vya roboti nchini China bado vinakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo ukosefu wa teknolojia muhimu, upanuzi wa maeneo ya matumizi ya teknolojia ya roboti, utaratibu wa sheria na kanuni zinazohusika bado unahitaji kukamilishwa. Bw. Miao Wei anasema:

    "China ni soko kubwa zaidi linalohitaji roboti duniani, na inakaribisha kampuni kutoka nchi mbalimbali kunufaika kwa pamoja na fursa hiyo ya maendeleo, kubeba kwa pamoja majukumu na kupata maendeleo kwa pamoja, ili kuhimiza viwanda vya roboti vipate maendeleo endelevu na yenye kiwango cha juu zaidi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako