• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vita vya kibiashara vya Marekani dhidi ya China vyaongeza hatari zinazokabili uchumi wa Latin Amerika

    (GMT+08:00) 2018-08-17 17:22:01

    Hivi karibuni kadiri vita vya kibiashara vya Marekani dhidi ya China vinavyozidi kupamba moto, ndivyo China inavyozidi kupanua soko la upande wa tatu. Nchi za Latin Amerika zikiwa nchi muhimu zinazotoa bidhaa zinazouzwa kwa wingi duniani, zina imani kubwa kunufaika kutokana na mgogoro wa kibiashara kati ya Marekani na China. Lakini wataalamu wanaonya kuwa, nchi za Latin Amerika zinapaswa kuwa macho kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya kujilinda kibiashara vya Marekani, na vita vyake vya kibiashara dhidi ya China.

    Sera ya kujilinda kibiashara inayotekelezwa na serikali ya Marekani ambayo inatoa kipaumbele maslahi ya Marekani si kama tu inailenga China bali pia imeharibu maslahi ya wenzi wake wa zamani zikiwemo nchi za Latin Amerika. Katibu mendaji wa Kamati ya uchumi wa nchi za Latin Amerika na Caribbean kwenye Umoja wa Mataifa Bibi Alicia Barcena ameeleza kuwa, Marekani imekwenda kinyume na kuharibu kanuni za biashara ya kimataifa pamoja na soko la dunia ili kujitafutia faida za kiuchumi na kuchukua hatua za kujilinda kibiashara, hatua ambayo imeharibu vibaya maendeleo ya uchumi wa nchi za Latin Amerika.

    Pia ameeleza kuwa China imekuwa mwenzi mkubwa wa pili wa biashara kwa Latin Amerika. Kutokana na mtazamo wa muda mrefu, vita vya kibiashara kati ya China na Marekani vitaharibu vibaya uchumi wa Latin Amerika. Anasema:

    "Tunaona kuwa hivi sasa China ina umuhimu mkubwa zaidi kuliko Marekani katika sekta ya uchumi na biashara. Kudumishwa kwa mgogoro wa kibiashara kati ya Marekani na China kutaathiri vibaya uchumi wa pande zote mbili. Iwapo uchumi na biashara ya China vitaathirika na kupunguza uagizaji wa bidhaa zinazouzwa kwa wingi, italeta msukosuko wa bei za bidhaa zinazouzwa kwa wingi duniani. Nchi za Latin Amerika zikiwa nchi zinazouza kwa wingi zaidi bidhaa za aina hiyo kwa China itapata na hasara kubwa zaidi."

    Bibi Barcena pia anasema kwamba hatua za kujilinda kibiashara za Marekani si kama tu zimeharibu soko la dunia nzima, bali pia zimeharibu utaratibu wa kawaida wa biashara, na kuleta migogoro mingi ya kibiashara ya makundi mengi ya kiuchumi duniani, ambayo ni changamoto kubwa zinazoyakabili mafungamano ya kiuchumi duniani. Anasema:

    "Hivi sasa China ikiwa moja ya nchi muhimu zinazowekeza moja kwa moja katika nchi za nje duniani. Inafanya juhudi za kufanya ushirikiano wa kimataifa wa "Ukanda mmoja, Njia moja", kuwekeza duniani na kuhimiza mawasiliano duniani. Wakati huo huo Marekani inajaribu kuzuia China kumiliki teknolojia muhimu kwa kuchukua hatua za kujilinda kibiashara, lakini China ina uwezo mkubwa wa kufanya utafiti yenyewe, na kupata matokeo mazuri kupitia ushirikiano wa kimataifa na vitendo vya kibiashara. Huu ni mwelekeo usioweza kuzuiliwa duniani. Wakati nchi zote duniani zinafanya juhudi za kujifungua kiuchumi, hatua yoyote ya kujilinda kibiashara haitakubaliwa na kamwe haitazuia mchakato wa mafungamano wa kiuchumi duniani."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako