• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Japan kuinua kiwango cha ushirikiano wa uchumi wa biashara

    (GMT+08:00) 2018-08-17 18:43:36

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang na mwenzake Shinzo Abe wa Japani wamezungumza kwa njia ya simu na kupeana pongezi katika maadhimisho ya miaka 40 tangu "Makubaliano ya Amani na Urafiki kati ya China na Japani" yasainiwe, na kusema nchi hizo mbili zitaimarisha ushirikiano wa kunufaishana na kuhimiza maendeleo ya utulivu na muda mrefu ya uhusiano kati yao.

    Sifa kuu ya uhusiano kati ya China na Japan uliodumu kwa miaka zaidi ya 40 ni kuwa uchumi na biashara za nchi hizo mbili hazitengani. Tangu mwaka 2007, China imekuwa mwenzi mkubwa zaidi wa biashara wa Japani. Mwaka 2017 thamani ya mauzo ya bidhaa za Japani kwa China imeweka rekodi na kufikia dola bilioni 134.5 za kimarekani, ambayo iliongezeka kwa asilimia 69 ikilinganishwa na ya mwaka 2005.

    Kwa kutazama siku za baadaye, uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Japani umetimiza muungano na kutarajiwa kuinuka kwa kiwango cha juu zaidi. Mwezi Machi mwaka huu, Idara ya biashara ya Japani JETRO ilitoa ripoti ya uchunguzi ikisema, bidhaa kuu zinazoagizwa kutoka China ni pamoja na simu za kisasa za mkononi, vifaa vya kushughulikia data vyenye skrini za kugusa, vifaa vya michezeo ya watoto, vifaa vya michezo na mavazi. Bidhaa zenye thamani zaida zimeanza kuchukulia hadhi kuu ya bidhaa zinazoagizwa kutoka China. Wateja wa Japani wameanza kupokea zama mpya ya kutumia vifaa vya kielektroniki vya China.

    Wakati huohuo, ukuaji imara wa uchumi wa China pia umeleta fursa kubwa ya biashara kwa kampuni za Japani na kushawishi mpango wao wa kimkakati duniani. Kutokana na mauzo ya magari nchini China kushikilia nafasi ya kwanza duniani kwa miaka 9 mfululizo, kampuni za magari za Japani zinapanga mkakati wa kuwekeza zaidi nchini China. Kwa mfano, ili kuendana na mkakati wa kubana matumizi ya nishati wa serikali ya China, kampuni ya Toyota ambayo ni moja kati ya kampuni kumi kubwa zaidi za magari duniani, imetangaza kuwa itatengeneza magari yanayotumia nishati ya umeme nchini China mwaka 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako