• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watanzania milioni 41 watumia zaidi ya trilioni 6 kulipia muda wa maongezi

    (GMT+08:00) 2018-08-17 20:15:14

    Watanzania milioni 41 wanaomiliki simu za mezani na mkononi wametumia zaidi ya Sh6 trilioni kwa ajili ya kulipia muda wa maongezi ndani na nje ya nchi na kutuma ujumbe mfupi (sms).

    Hata hivyo, kiwango hicho kinaweza kupungua kutokana na baadhi ya mitandao ya simu kuwa na vifurushi vya maongezi na sms ambavyo ni kwa ajili ya promosheni ya kuvutia wateja zaidi. Kiasi hicho cha matumizi kilirekodiwa kwenye robo ya pili ya mwaka iliyoishia Juni ni kikubwa ikilinganishwa na Sh4.8 trilioni zilizotumika katika kipindi kama hicho mwaka jana.

    Kuongezeka kwa kiasi hicho ni kutokana na ongezeko la muda wa kupiga simu (dakika) na idadi ya ujumbe mfupi. Gharama nyingi isipokuwa kupiga simu nje ya nchi zilipungua katika vipindi hivyo vilivyofanyiwa uchambuzi. Ripoti ya mawasiliano kwa robo ya pili ya mwaka iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), inaonyesha mpaka sasa jumla ya watu milioni 41.8 wanatumia simu tofauti na kipindi kama hiki mwaka uliopita ambapo watumiaji walikuwa milioni 40.3. Katika kipindi kilichoishia Juni 30, Sh4.4 trilioni zilitumika kama gharama ya muda wa maongezi, huku Sh1.7 zikiwa ni gharama ya kutuma ujumbe mfupi wa maandishi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako