• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • ATCL kuanza safari kuanzia mwishoni mwa mwezi huu

    (GMT+08:00) 2018-08-17 20:15:39

    Shirika la Ndege nchini Tanzania (ATCL) litaanza kufanya safari za kwenda Entebbe, Uganda na Bujumbura, Burundi kuanzia mwishoni mwa mwezi huu. Kuanza kwa safari hizo ni jitihada za shirika hilo kujitanua kibiashara baada ya kuendelea kufanya vyema katika soko la ndani.

    Ndege zitakazofanya safari hizo ni Bombardier Dash 8 Q400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja. Akizungumza na radio China Kimataifa, Mkurugenzi Mtendaji na Mtendaji Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi, amesema kuwa safari ya kwenda Entebbe zitaanza Agosti 26, huku za Bujumbura zikianza Agosti 30, mwaka huu.

    Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa ATCL, Josephat Kagirwa, amesema safari hizo zitakuwa zikifanyika mara tatu kwa wiki. Kwa mujibu wa Kagirwa, safari za kutoka Dar es Salaam kupitia Kilimanjaro kwenda Entebbe zitakuwa zikifanyika siku za Jumanne, Ijumaa na Jumapili na safari za kutoka Dar es Salaam kupitia Kigoma kwenda Bujumbura zitakuwa zikifanyika siku za Jumatatu, Jumatano na Jumapili.

    Ndege hizo zitakuwa zikianza safari zake kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam saa 3:30 asubuhi, lakini ndege inayoenda Entebbe itakuwa ikirejea Dar es Salaam saa 8:50 mchana na ile inayoenda Bujumbura itakuwa ikirejea Dar es Salaam saa 10 jioni. Kagirwa aliongeza kuwa kwenye kila ndege kutakuwa na daraja la biashara na daraja la kawaida ambapo kwenye daraja la biashara kutakuwa na viti sita na viti vingine 70 vilivyosalia ni kwa ajili ya daraja la kawaida.

    Amesema ATCL imeweka bei nafuu kwa wateja wao watakaokuwa wakisafiri na ndege hizo kwenda Entebbe na Bujumbura, lakini pia utaratibu wa kupata tiketi ni ule ule wa ama kufika kwenye ofisi za ATCL, kukata kwa njia ya mtandao au kupitia kwa mawakala wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako