• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya na Uingereza kushirikiana katika biashara

    (GMT+08:00) 2018-08-17 20:15:54

    Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May anatarajiwa kutembelea Kenya mwishoni mwa mwezi huu ikiwa ni ziara inayolenga kuboresha biashara kati ya Kenya na Uingereza. Afisa mkuu katika wizara ya mambo ya nje Amesema ziara ya May inalenga kupiga jeki ajenda kuu za Rais Kenyatta. Ajenda hizo ambazo ni, kuimarisha sekta ya afya ili kila mwananchi apate matibabu bora, ujenzi wa viwanda na kampuni ili kutatua ukosefu wa ajira hasa kwa vijana, makazi nafuu na bora, na kuangazia usalama wa chakula, zinalenga kuhakikisha rais ameacha rekodi bora ya utendakazi wakati akistaafu 2022. Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Bi Monica Juma amesema rais anapania kuona Kenya inashirikiana kwa karibu na Uingereza ili kuimarisha sekta ya biashara kati ya mataifa hayo mawili. Hii ina maana kuwa Kenya inatarajia makuu kustawi kibiashara kutokana na ziara ya Waziri May. Ziara ya May inatarajiwa kuimarisha uchumi wa Kenya na Uingereza, ili kuona vijana wanapata nafasi za kazi. Uingereza inajulikana duniani kwa kilimo cha mimea kama mahindi, ngano, mboga, matunda, maharagwe, miongoni mwa mingine. Ziara ya May Barani Afrika ni ya kwanza tangu amrithi mtangulizi wake David Cameron Julai 2016.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako