• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Li Keqiang ampongeza Bw. Imran Khan kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mpya wa Pakistan

    (GMT+08:00) 2018-08-18 16:02:33

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amempongeza Bw. Imran Khan kwa kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mpya wa Pakistan.

    Katika salamu zake za pongezi, Bw. Li amesema China na Pakistan ni wenzi wa ushirikiano wa kimkakati, na uhusiano kati ya nchi hizo mbili umehimili mtihani wa muda na mabadiliko ya hali ya kimataifa, na unasonga mbele kwa utulivu. Amesema katika miaka ya hivi karibuni, China na Pakistan zimezidi kuaminiana kisiasa, na kushirikiana vizuri kuhusu ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na ujenzi wa ushoroba wa kiuchumi wa China na Pakistan, jambo ambalo limezipa manufaa halisi nchi hizo mbili na wananchi wake.

    Ameongeza kuwa anatarajia Bw. Khan ataendelea kukuza uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na anapenda kufanya kazi pamoja na Bw. Khan kuendeleza urafiki wa jadi kati ya China na Pakistan. Pia kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana katika sekta mbalimbali na kufanya juhudi kujenga Jumuiya yenye hatma ya pamoja ya binadamu kati ya China na Pakistan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako