Kituo cha Televisheni cha Al Jazeera cha Qatar kimeripoti kuwa aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Kofi Annan amefariki dunia leo, akiwa na umri wa miaka 80.
Bw. Annan, alizaliwa Kumasi nchini Ghana. Katika awamu mbili za uongozi wake kuanzia tarehe Mosi, Januari mwaka 1997 hadi tarehe 31, Disemba mwaka 2006, alisimamia masuala kadhaa ikiwemo usalama wa umma, umoja wa kimataifa, haki za binadamu na utawala wa kisheria, na ulinzi wa thamani na mamlaka ya maadili ya Umoja wa Mataifa. Pia alisaidia kuimarisha hadhi ya Umoja wa Mataifa katika mambo ya kimataifa na kuhimiza maendeleo ya utaratibu wa pande nyingi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |