• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uwekezaji wa nchi za nje nchini China waongezeka

    (GMT+08:00) 2018-08-20 16:48:45

    Takwimu mpya zilizotolewa na wizara ya biashara ya China zinaonesha kuwa, idadi ya kampuni mpya zenye uwekezaji kutoka nje zilizoanzishwa katika miezi 7 iliyopita nchini China ilikuwa 35,239, ambalo ni ongezeko la asilimia 99.1 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu, na matumizi halisi ya uwekezaji wa nchi za nje ni dola bilioni 72.3 za kimarekani. Wakati huo huo uwekezaji kutoka nchi za nje umeingia zaidi kwenye sekta za teknolojia ya hali ya juu, haswa viwanda vya utengenezaji wa vifaa vya mawasiliano ya habari, kompyuta, na vifaa vya matibabu.

    Je, wakati China inapokabiliwa na vita ya biashara iliyoanzishwa na Marekani na hali ya kutatanisha ya uchumi wa kimataifa, kwa nini uwekezaji wa nchi za nje unaoingia nchini China unaongezeka? Wachambuzi wanaona kuna sababu tatu.

    Kwanza, China imeboresha mazingira ya biashara kwa hatua mfululizo, na kupunguza vizuizi kwa uwekezaji kutoka nje hatua kwa hatua. Kwa mujibu wa kiwango cha vizuizi kwa uwekezaji kilichokadiriwa na Shirika la Ushirikiano na Maendeleo ya Uchumi Duniani OECD, nafasi ya China imeshuka kwa ngazi nne tangu mwaka 2015, na hali ambayo inaonesha kuwa mazingira ya uwekezaji nchini China inaboreshwa siku hadi siku.

    Pili, China imejitokeza katika ukamilifu wa mtandao wa sekta za uchumi, uwezo wa uzalishaji, na ukubwa wa soko, na kuweza kukidhi mahitaji ya uzalishaji wa kampuni za nje za nje kwa pande zote. Kwa hivyo, tangu vita ya kibiashara kati ya China na Marekani ianze mwezi Machi, baadhi ya kampuni za nchi za nje zikiwemo BMW na Tesla zimeongeza uwekezaji nchini China. Mbali na hayo, soko kubwa ambalo bado linakua kwa kasi kubwa nchini China linavutia uwekezaji kutoka nchi za nje.

    Tatu, China ina nia na hatua halisi za kufungua mlango zaidi. China inajitahidi kujenga majukwaa mapya ya ushirikiano ikiwemo "Ukanda Mmoja na Njia Moja" na "China na Umoja wa Nchi za Asia ya Kusini Mashariki", kuongeza ushirikiano wa BRICS, na kulinda utaratibu wa biashara wa pande nyingi.

    Huu ni mwaka 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango. Mwaka jana kwenye mkutano wa DAVOS, Rais Xi Jinping alitangaza kuwa China itavutia uwekezaji wa dola bilioni 600 kutoka nchi za nje kati ya mwaka 2017 na 2021. Katika siku zijazo, China itaendelea kupunguza vizuizi kwa uwekezaji kutoka nchi za nje, na kuboresha mazingira ya kibiashara, ili kuziwezesha kampuni za nchi za nje kupata mafanikio zaidi nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako