• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Salvador zaanzisha uhusiano wa kibalozi

    (GMT+08:00) 2018-08-21 19:16:19

    Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi na mwenzake wa Salvador Bw. Carlos Castaneda wamesaini azimio la pamoja la kuanzisha uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili mjini Beijing.

    Azimio hilo limesema, kwa mujibu wa maslahi na nia ya watu wa nchi hizo mbili, tangu kusainiwa kwa azimio hilo, China na Salvador zitaanzisha uhusiano wa kibalozi. Nchi hizo mbili zimekubali kuheshimiana uhuru na ukamilifu wa ardhi, kutoshambulia, kutoingilia kwenye mambo ya ndani na kushirikiana kwa usawa na amani. Pia Salvador inafuata sera ya China moja. Serikali ya China ni serikali pekee halali inayowakilisha China. Taiwan ni sehemu isiyotengeka ya China. Serikali ya Salvador imeahidi kusitisha na kuacha uhusiano rasmi na Taiwan.

    Habari zinasema, Rais Salvador Sanchez Ceren wa Salvador amesema, anaamini hatua hiyo ni sahihi na kufuata sheria ya kimataifa, kanuni ya uhusiano wa kimataifa na mwelekeo wa maendeleo ya kisasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako