• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka, Kufuzu Afcon-U17: Tanzania na Rwanda zafuzu nusu fainali

  (GMT+08:00) 2018-08-22 10:18:34

  TIMU ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Tanzania, Serengeti Boys imefanikiwa kumaliza kwenye nafasi ya kwanza ya Kundi A ya michuano ya kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA AFCON Qualifier) baada ya ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Rwanda (Amavubi Juniors) jana jioni mjini Dar es Salaam.

  Kwa ushindi huo, Tanzania inafikisha pointi tisa baada ya kucheza mechi tatu na kushinda zote, wakati Rwanda inamaliza nafasi ya pili na zote tayari zimefuzu Nusu Fainali, lakini Burundi na Sudan zikiaga.

  Tanzania na Rwanda sasa zinasubiri matokeo ya mechi za kundi B zitakazopigwa leo, Uganda dhidi ya Djibouti, na Ethiopia dhidi ya Kenya.

  Michuano ya Mataifa ya Afrika kwa vijana inatarajiwa kuanza Mei 12 hadi Mei 26 mwaka 2019 nchini Tanzania.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako