• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Beijing iko tayari kwa mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2018-08-22 17:09:03

    Mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika utafanyika hapa Beijing kuanzia tarehe 3 hadi 4, mwezi Septemba. Mjumbe wa taifa ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema, huu ni mkusanyiko mwingine wa familia kubwa ya China na Afrika, na pia ni mkutano mkubwa zaidi wa mwaka huu nchini China. Sasa mji wa Beijing uko tayari, na utawapokea marafiki wa China kutoka nchi mbalimbali za Afrika kwa ukarimu.

    Kwa mujibu wa ajenda iliyoamuliwa na China na Afrika, ufunguzi wa mazungumzo kati ya viongozi na wajumbe wa viwanda na biashara kutoka China na nchi za Afrika, pamoja na mkutano wa 6 wa wanaviwanda wa China na Afrika utafanyika asubuhi ya tarehe 3, na mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika utafunguliwa alasiri ya siku hiyo. Bw. Wang Yi anasema,

    "Rais Xi Jinping wa China atatoa hotuba muhimu, kufafanua mawazo na mapendekezo mapya ya kuimarisha uhusiano kati ya China na Afrika, na kutangaza hatua mpya za kuhimiza ushirikiano halisi ambazo zitazingatia zaidi maendeleo ya sekta za uchumi, miundombinu, biashara na uwekezaji, maendeleo ya nguvukazi, shughuli za elimu, sayansi utamaduni na afya, uhifadhi za mazingira, amani na usalama."

    Mkutano wa majadiliano kati ya viongozi wa China na nchi za Afrika utafanyika tarehe nne. Viongozi hao watabadilishana maoni kuhusu maendeleo ya uhusiano kati ya nchi zao na masuala ya kimataifa na kikanda wanayoyafuatilia. Mkutano huo pia unatarajia kupitisha Azimio la Beijing kuhusu kujenga jumuiya ya karibu zaidi yenye mustakabali wa pamoja ya China na Afrika, na mpango wa harakati ya Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika.

    Msaidizi wa waziri wa mambo ya nje ya China Bw. Chen Xiaodong amesema kauli mbiu ya mkutano huo ni "ushirikiano na mafanikio ya pamoja, kujenga kwa pamoja jumuiya ya karibu zaidi yenye mustakabali wa pamoja ya China na Afrika". Anasema, 

    "Mkutano huo wa kilele utadhihirisha zaidi malengo ya kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya China na Afrika, na kutoa hatua mpya za kukuza ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika sekta mbalimbali, na kusaidia Afrika kupata maendeleo endelevu kwa kujiamulia.

    Bw. Wang Yi amesema, katika miaka 18 iliyopita tangu kuanzishwa kwa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, pande hizo mbili zimeshikilia kanuni ya kushauriana, kujijenga kwa pamoja na kunufaishana. Baraza hilo limekuwa bendera ya kuongoza ushirikiano wa kimataifa kwa Afrika, na kuinua kiwango cha ushirikiano kati ya nchi za kusini. Amesema mkutano huo wa kilele utahimiza ushirikiano kati ya China na Afrika uwe wa kiwango cha juu zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako