Mpango huo ambao unashirikisha kampuni ya Huawei unalenga kutatua changamoto mbalimbali kupitia wataalamu wake duniani ikiwa ni pamoja na kutumia nyenzo za kitaalamu.
Mradi huo unaofahamika kama "Seeds for the Future" ulianzishwa miaka mitatu iliyopita ambapo jana ulizinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei,Gao Mengdong alisema kampuni yake ina wajibu wa kutoa huduma kimataifa.
Alisema Huawei itatoa mafunzo ya wakufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),Taasisi ya Ufundi Dar es Salaam (DIT),na Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA),ili kuwapa ujuzi katika kozi mbalimbali za ICT.
Aidha Mengdong alisema anaamini kuwa hii italeta mabadiliko chanya katika maendeleo na ukuaji wa uchumi nchini Tanzania.
Alisema kila mwaka mpango huo hutoa fursa kwa wanafunzi 10 wa vyuo vikuu kutoka Tanzania kwenda Beijing,China kutembelea shughuli mbalimbali za Huawei katika makao makuu yake mjini Shenzhen.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |