• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Beckham kutunukiwa tuzo ya heshima ya rais wa UEFA

  (GMT+08:00) 2018-08-23 09:45:05

  Kiungo na nahodha wa zamani wa Timu ya England, David Beckham atazawadiwa tuzo ya Rais wa UEFA kwa mchango wake kwenye soka sambamba na kuutangaza mchezo huo dunia nzima.

  Beckham aliwahi kuchezea Timu za Manchester United, La Galaxy, Real Madrid, AC Milan na Paris St-Germain katika kipindi cha miaka 20 ya uchezaji wake.

  Shirikisho hilo la Soka la Ulaya pia limepongeza jitihada za kibinidamu zisizochoka za mchezaji huyo wa zamani.

  Tuzo hiyo ambayo inatambua mafanikio ya mfano wa kuigwa kwenye soka la kulipwa na sifa binafsi za mtu zinazopaswa kuigwa imewahi kunyakuliwa na mkali wa zamani wa Barcelona, Johan Cruyff, nyota wa England Bobby Charlton na Bobby Robson, kinara wa Ujerumani, Franz Beckenbauer, na Paolo Maldini wa Italia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako