Mradi huu unalenga kuongeza teknolojia kwa ajili ya mageuzi ya kilimo Afrika katika mnyororo wa thamani wa maharage,machungwa na viazi vitamu.
Mradi huu,katika nchi 12 barani Afrika,unalenga kusaidia mkakati wa benki ya AfDB wa kulisha Afrika ili bara hilo liweze kupunguza uagizaji mkubwa wa chakula. Hii itafanikishwa kupitia upigaji jeki wa uwezo wa kilimo Afrika.
Mtafiti Mkuu katika Bodi ya Kilimo ya Rwanda ,Augustin Musoni, alisema kuwa mpango huo utawanufaisha watu zaidi ya 100,000 watakaowekwa katika makundi ya kaya 30,000 nchini Rwanda.
Alisema watakaonufaika ni wale walio katika mnyororo wa thamani wa baadhi ya mimea kwa kupatiwa teknolojia muafaka za uzalishaji chakula.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |