• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Nyota wa Serengeti Boys ahitajika Manchester United

  (GMT+08:00) 2018-08-24 09:18:19

  Baada ya kuonesha kipaji maridhawa kwa mechi kadhaa alizochezwa, imeelezwa kuwa uongozi wa Manchester United kupitia wakala wake umeanza harakati za kuwania saini ya mshambuliaji, Kelvin John anayekipiga timu ya taifa ya vijana (U17), Serengeti Boys.

  John ambaye yupo katika mashindano ya CECAFA na timu hiyo, aliibuka kidedea katika mchezo wa mwisho dhidi ya Rwanda kwa kufunga mabao matatu pekee katika ushindi wa mabao 4-0.

  Taarifa kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imeeleza kuwa tayari mazungumzo yameshaanza baina yake na wakala huyo kwa ajili ya kumsajili John.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako