• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maofisa wa Kebs kukaguliwa upya

    (GMT+08:00) 2018-08-24 18:34:21

    Waziri wa Viwanda wa Kenya Bw Peter Munya amesema maafisa wa Shirika la Kukadiria Ubora wa Bidhaa (KEBS) watakaguliwa upya.

    Waziri huyo amesema kulikuwa na mipango ya kutekeleza marekebisho KEBS na kuongeza idadi ya wafanyikazi na kuwachunguza upya maafisa wa sasa.

    Bw Munya alitoa agizo kwa bodi kubuni mikakati ya kuchunguza upya maafisa hao, katika zoezi litakaloanza mara moja.

    Kulingana na waziri huyo, maafisa wa KEBS na maafisa wengine wa utekelezaji ni sehemu ya changamoto ilioko katika vita dhidi ya bidhaa ghushi na za magendo.

    Maafisa wakuu wa KEBS akiwemo meneja mkurugenzi Charles Ongwae Juni walishtakiwa kwa uagizaji wa mbolea ya ubora wa chini na uenezaji wa stempu feki za KEBS.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako