• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka: Uganda washinda ubingwa wa CECAFA AFCON U-17, Wafuzu michuano ya Afrika mwakani

  (GMT+08:00) 2018-08-27 10:25:43

  UGANDA wameendelea kudhihirisha ubora wao katika soka ngazi ya kanda baada ya kutwaa ubingwa kwenye michuano ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 kwa ukanda wa Afrika Mashariki (CECAFA AFCON U-17 Qualifiers 2019) kufuatia ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Ethiopia jana mjini Dar es Salaam, nchini Tanzania.

  Kwa ushindi huo, Uganda sasa wamefuzu kushiriki michuano ya vijana ya AFCON U-17 mwezi mei mwaka 2019, Lakini Tanzania ambao walishika nafasi ya tatu kwenye mashindano hayo wanafuzu moja kwa moja kwa kuwa wao ndiyo wenyeji.

  Kwa ubingwa huo, Rais wa CAF Ahmed Ahmed aliwakabidhi kombe la ubingwa Uganda. Lakini Tuzo ya mchezaji bora ilikwenda kwa Kevin Pius wa Tanzania, Mfungaji bora Mintesnot Endrias wa Ethiopia, golikipa bora Alzar Mako wa Ethiopia pia, na timu iliyotwaa tuzo ya mchezo wa kiungwana ni Tanzania.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako