• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wa Afrika na wa China wanatarajia ushirikiano kuendelea kwenye mjadala wa FOCAC

    (GMT+08:00) 2018-08-27 20:04:55

    Wataalamu wa Kiafrika na wa China wanatarajia ushirikiano kuendelea kuongezeka kutokana na mkutano wa Baraza la Ushirikiano wa China na Afrika takaofanyika Septemba 3-4 huko Beijing.

    Mkutano wa FOCAC wa Beijing utaandaliwa chini ya maudhui ya, "China na Afrika: Kuelekea na jumuiya yenye nguvu zaidi na ushirikiano wenye kunufaisha pande zote kwa usawa.

    Akizungumza na waandishi wa habari, Balozi wa China nchini Ethiopia Tan Jian alisema mkutano huo utakuwa tukio la kihistoria la kukusanya familia kubwa kati ya China na nchi za Afrika, kufuatia mkutano uliopita uliofanyika mwaka 2015 huko Johannesburg, Afrika Kusini.

    Naye Naibu Waziri wa Fedha na Ushirikiano wa Uchumi wa Ethiopia Admasu Nebebe, alisema mkutano huo wa FOCAC unatarajiwa kujadili kwa kina nja za kuimarisha ushirikiano wao, hasa katika sekta za mabadiliko ya kilimo, maendeleo ya viwanda, maendeleo ya miundombinu na sayansi na teknolojia.

    Mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika, Rais Paul Kagame wa Rwanda, atakuwa mmoja wa wasemaji wanne katika sherehe ya ufunguzi wa FOCAC Septemba 3.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako