• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • BoT yapunguza riba tena Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-08-27 20:05:14

    Wananchi wa kawaida na wafanyakazi watapata afueni ya kukopa katika benki mbalimbali nchini huku riba zikitarajiwa kupunguzwa tena na muda wa kurudisha mikopo kuongezwa.

    Wafanyabiashara wadogo, wananchi wa kawaida, wafanyakazi na sekta binafsi za biashara zitapata fursa ya kukopa na sifa ya kukopesheka baada ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT)kupunguza riba kwa benki nchini kutoka asilimia tisa hadi saba.

    Punguzo hilo la riba linazipa benki fursa ya kukopa na kurudisha kwa riba ndogo zaidi.

    Barua ya Naibu Gavana wa BoT anayesimamia sera za uchumi na fedha (EFP), Dk Yamungu Kayandabila imesema punguzo hilo la riba litaanza rasmi Agosti 27 na litaendelea hadi yatakapofanyika mapitio mapya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako