• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Marufuku ya kuuza parachichi za Kenya nchini Afrika Kusini yaondolewa

    (GMT+08:00) 2018-08-27 20:05:32

    Kenya sasa inaweza kuuza nje ya parachichi nchini Afrika Kusini baada ya miaka 11 ya soko kufungwa kutokana na hatari ya nzi wa matunda.

    Hii inafuata mazungumzo ya kufana yanayoongozwa na mashirika ya serikali ikiwa ni pamoja na wizara zinazosimamia Kilimo na Biashara.

    Serikali ya Afrika Kusini iliweka marufuku kwa parachichi kutoka Kenya mwaka 2007 kutokana na uwepo wa wadudu hao.

    Nzi hao wanaaminika kutokea barani Asia na kuripotiwa kwanza nchini Kenya mwaka na kisha kuenea kwa maeneo ya uzalishaji wa matunda nchini humo.

    Kwa sasa, kuna zaidi ya ekari 112,107 zilizopandwa parachichi nchini Kenya lakini wizara ya kilimo inapanga kuongeza hadi ekari 200,210 ifikapo mwaka 2022.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako