• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TPA KUENDELEZA BANDARI KIUSHOROBA

    (GMT+08:00) 2018-08-28 20:19:23

    MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imejipanga kuendeleza bandari kiushoroba kuongeza ufanisi wa huduma na kuzisogeza karibu zaidi na wateja.

    Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Deusdedit Kakoko amesema, ili kuweza kupata manufaa hayo, bandari hizo hazina budi kwenda sambamba na maendeleo ya ushoroba ndani ya nchi na kieneo.

    Amesema kwa upande wa ushoroba wa Kati Kaskazini (Mwanza), imelenga uboreshaji wa bandari ya ziwa Victoria na ujenzi wa bandari kavu ya Fela- Mwanza na utasogeza huduma za bandari kwa wateja wa Kanda ya Ziwa na nchi jirani za Uganda na Sudan Kusini.

    Amesema TPA inashirikiana na TAZARA ili kuhakikisha huduma za reli ya TAZARA zinarejea angalau kwa kiwango cha kuridhisha ili kuhudumia wateja wa Kusini Magharibi mwa Tanzania, sambamba na mpango wa kujenga bandari Kavu ya Inyala-Mbeya ili kuhudumia nchi jirani za DRC, Malawi na Zambia.

    Aidha amesema hivi sasa wanaendelea na maboresho ya bandari ya Mtwara ili kuhudumia wateja wa kusini mwa Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako