• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jukwaa la biashara la kielektroniki la Amanbo larahisisha biashara kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2018-08-29 08:46:47

    Mwezi Desemba mwaka 2015, kwenye mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC uliofanyika Johannesburg, Afrika Kusini, rais Xi Jinping wa China alitangaza kuinua kiwango cha uhusiano kati ya China na Afrika kuwa uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote, na kutoa mipango 10 mikubwa ya ushirikiano katika sekta za viwanda, kilimo, miundombinu, fedha, maendeleo yasiyochafua mazingira, kurahisisha biashara na uwekezaji, kuondoa umaskini na kuwanufaisha watu, afya, utamaduni, amani na usalama. Katika kipindi cha leo, utasikiliza ripoti ya sita "Jukwaa la biashara la kielektroniki la Amanbo linavyohimiza na kurahisisha biashara kati ya China na Afrika".

    Tovuti za biashara ya kwenye mtandao ikiwemo Alibaba, Taobao, JD.com sio jambo geni kwa wateja wa China. Manunuzi kupitia mtandao wa Internet yamefikia pande mbalimbali za maisha ya watu wa China. Jukwaa la biashara la kielektroniki la Amanbo la China pia limejitokeza nchini Kenya, na limekuwa chaguo jipya kwa wakenya kufanya biashara na kununua vitu.

    "Mambo, hapo ni ofisi ya Amanbo nchini Kenya, mimi Karen nitakuhudumia, nitakusaidiaje? Unataka ngapi? Sawa, kwanza tafadhali ingia katika akaunti yako."

    Meneja wa kituo cha jukwaa la biashara la kielektroniki la Amanbo nchini Kenya Bibi Karen Mokeira Obwaya, anajibu maswali ya wateja, kila siku anaweza kupokea wateja zaidi ya mia moja wanaokuja kutembelea huku akiwasaidia wafanyabiashara wa Kenya wanaotaka kununua bidhaa kutoka China, na wateja wa kawaida wa huko kumaliza usajili, matumizi na biashara kwenye jukwaa hilo. Anaona kuwa jukwaa la biashara la kielektroniki lina mvuto mkubwa sana kwa wakazi wa huko, ambalo kasi yake, ufanisi na urahisi wake unasifiwa sana. Anasema,

    Tangu jukwaa la biashara la kielektroniki la Amanbo litolewe mwaka 2015, idadi ya watumiaji wake imezidi laki moja huku idadi ya wafanya biashara wadogo na wa wastani ikizidi elfu 30. Mwaka huu, thamani ya biashara kupitia jakwaa hilo inatarajiwa kuzidi dola milioni 30 za kimarekani. Meneja mkuu wa kituo cha jukwaa la biashara la kielektroniki la Amanbo nchini Kenya. Bw. Yin Yingbin, anasema mafanikio yaliyopatikana Amanbo ndani ya muda mfupi, yanatokana na uzoefu na utekelezaji wake katika miaka minane iliyopita barani Afrika na mnyororo wa kitekolojia wa biashara za kielektraoniki kati ya China na Afrika, unaofaa hali halisi ya Afrika. Anasema,

    "Kwa kutegemea mtindo maalumu wa OSO wa Amanbo (online+ social+ offline), kupitia jukwaa la Internet, jumba la maonesho nje ya Internet na maghala ya nje ya China pamoja na wafanyakazi wa huko na wenzi wa soko la Amanbo, tumejenga jukwaa la biashara la kielektroniki la B2B2C (Watoaji bidhaa kwa kampuni, kampuni kwa wateja). Hivyo, wafanya biashara wanaweza kuuza bidhaa kwa jumla au rejareja, kufanya biashara za kuvuka mpaka ama katika soko la huko kupitia jukwaa letu."

    Bw. Abdikadir Ahmed Hassan ni mwenye duka jijini Nairobi anayetumia Amanbo kwa miaka miwili. Duka lake linauza bidhaa za kielektroniki za chapa mbalimbali ikiwemo televisheni, vipaza sauti na simu za mkononi, ambazo zote ni Made in China. Bw. Hassan alikuwa na tatizo la kununua bidhaa za China zenye sifa nzuri na bei nafuu: ameshindwa kununua bidhaa kutoka China kutokana na kutolewa lugha ya kichina na gharama ya juu, ambapo pia bei ni ya juu na aina ni za chache akinunua kutoka wauzaji wa bidhaa nchini Kenya. Alipata fursa ya kutembelea jumba la maonesho la Amanbo, na kuamua kujisajili kwenye jukwaa hilo na kuanza kununua bidhaa kutoka jukwaa hilo.

    Bw. Hassan amesema, jukwaa la biashara la kielektroniki linakua kwa kasi, watu wanaanza kupokea kitu hicho kipya, huku wafanyabiashara wengi wadogowadogo na wa wastani kama yeye wakijaribu kuuza bidhaa kwenye jukwaa hilo. Ingawa hivi sasa wateja wengi wananunua bidhaa kwenye maduka halisi, idadi ya wanaonunua kupitia mtandao wa Internet pia inaongezeka. Ana imani na maendeleo ya jukwaa la biashara la kielektroniki. Anasema,

    "Ukuaji wa mtandao wa Internet nchini Kenya pia unahimiza maendeleo ya jukwaa la biashara la kielektroniki. Katika miezi sita iliyopita tumepata rekodi nzuri ya mauzo kwenye Internet, naamini kuwa katika miaka kadhaa ijayo, jukwaa la biashara la kielektroniki litaendelea kwa kasi sana."

    Sio tu kuuza bidhaa za China nchini Kenya, ili kuwasaidia wafanyabiashara kuuza bidhaa za huko nchini China, jukwaa la Amanbo pia limefungua tovuti ya mauzo ya bidhaa za Afrika. Mkurugenzi mtendaji mkuu wa jukwaa hilo Bw. Liao Xuhui amesema, hatua hiyo itawasaidia wafanyabiashara wengi zaidi kunufaishwa na ukubwa wa soko la China. Anasema,

    "Ni vigumu kwa wafanya biashara kuingia nchini China. Ingawa wanajua China ina soko kubwa sana, lakini hawana njia ya kuanzisha biashara na China. Licha ya kuuza bidhaa kwa ujumla kwa China, wafanyabiashara wadogowadogo na wa wastani, wanakosa njia ya kuingia katika soko la China. Sasa tumetengeneza tovuti ya mauzo ya bidhaa ya Afrika, licha ya kusamehe gharama za matumizi ya tovuti hiyo, pia tumejenga kituo cha maonesho ya bidhaa za Afrika huko Shenzhen kinachoitwa "Kuonja Afrika", ili wateja wa China waweze kuangalia moja kwa moja bidhaa hizo. Mtindo huo umepongezwa na serikali, vyama vya wafanyabiashara, tuna uwezo mkubwa wa kupanua soko hilo. "

    Mwezi Desemba mwaka 2015, kwenye mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC uliofanyika Johannesburg, Afrika Kusini, rais Xi Jinping wa China alitangaza kuinua kiwango cha uhusiano kati ya China na Afrika kuwa uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote, na kutoa mipango 10 mikubwa ya ushirikiano. Mpango wa urahisishaji wa biashara kati ya China na Afrika ambao ni moja ya mipango hiyo kumi, umependekeza kuhimiza ushirikiano wa biashara za kielektroniki, kutia moyo kampuni za China kuanzisha ushirikiano wa "Internet Plus" na bara la Afrika, ili kuifanya Afrika kunufaika na teknolojia za habari na uchumi wa data kubwa.

    Jukwaa la biashara la kielektrokini la Amanbo likiwa nguvu kubwa ya kuhimiza urahisishaji wa biashara za kielektroniki limepata uungaji mkono kutoka serikali za China na Kenya. Wizara ya viwanda na teknolojia ya habari ya China imeiweka Amanbo kuwa mradi muhimu wa ushirikiano na Afrika, na kuialika kushiriki kwenye mradi wa barabara kuu ya habari ya China na Afrika. Wizara ya mambo ya nje na wizara ya biashara ya China pia zimetoa uungaji mkono mkubwa kwa jukwaa hilo, ambao ni pamoja na utoaji wa idhini na kuisadia kuvutia mitaji na uwekezaji. Wakati huohuo, Jukwaa hilo la Amanbo pia limepata uungaji mkono kutoka wizara ya viwanda na biashara ya Kenya, wizara ya mawasiliano ya habari ya Kenya, kamati ya kuhimiza mauzo ya bidhaa nje na idara ya kuhimiza uwekezaji ya Kenya, huku likisaini makubaliano ya ushirikiano na jumuiya kubwa zaidi ya viwanda na biashara ya Kenya KNCCI, chama cha wauzaji na waagizaji wa bidhaa kutoka nje cha Kenya, chama cha maua, kokwa na ngozi. Naibu mwenyekiti wa Chama cha KNCCI Bw. James Ndungu Mureu amesema jukwaa la biashara la kielektroniki la Amanbo limewasaidia wafanyabiashara wa Kenya kutatua tatizo la kufanya biashara na China, na chama hicho kitasaidia kwa pande zote maendeleo ya Amanbo nchini Kenya. Mkurugenzi mtendaji mkuu wa Amanbo Bw. Liao amesema, ana imani na maendeleo ya siku za baadaye za jukwaa la biashara la kielektroni kati ya China na Afrika, ambayo sio tu ni mahitaji ya maendeleo ya bara la Afrika, bali pia ni mahitaji ya pande zote mbili za biashara za China na Afrika.

    "Katika miaka saba au nane iliyopita, karibu nusu kati ya nchi 20 zenye ongezeko la kasi l pato la taifa GDP duniani ni nchi za Afrika. Uhusiano kati ya China na Afrika umekuwa wa karibu zaidi baada ya mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC uliofanyika Johannesburg, hivyo biashara ya kielektroniki ikiwa mtindo mpya wa biashara wenye ufanisi mkubwa zaidi imefuatiliwa sana na jumuiya ya kimataifa, na kutambuliwa na soko. Mbali na hayo, soko pia lina mahitaji. Kufuatia maendeleo ya teknolojia na ujenzi wa miundombinu, msingi wa maendeleo ya biashara ya kielektroniki pia umetimizwa. Ustawi wa Afrika, maendeleo ya ushirikiano kati ya China na Afrika na mahitaji ya soko pamoja na ukuaji wa teknolojia vyote vimetia nguvu ya kudumu kwa maendeleo ya Afrika."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako