• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka, Klabu Bingwa Afrika: Horoya FC ya Guinea, yafuzu robo fainali kwa mara ya kwanza

  (GMT+08:00) 2018-08-29 10:51:16

  Baada ya mechi za mwisho za hatua ya makundi za klabu bingwa Afrika zilizochezwa jana, Al Ahly ya Misri, na Esperance ya Tunisia za kutoka kundi A, TP Mazembe ya DRC, na Entente Setif ya Algeria za kundi B, Wydad Casablanca ya Morocco na Horoya AS ya Guinea kundi C, Etoile Du Sahel ya Tunisia na Primeiro De' Agosto ya Angola, ndizo timu pekee zilizofuzu hatua ya robo fainali kutokana na kuwa na wingi wa pointi kuliko timu zingine katika makundi hayo.

  Katika mechi hizo za mwisho kulishuhudiwa mabingwa wa mwaka 2016, Mamelodi Sundowns kutoka Afrika Kusini wakishindwa kutumia fursa pekee iliyokuwa imebaki walipocheza nyumbani mjini Pretoria dhidi ya Horoya AS ya Guinea na kutoka sare ya bila kufungana.

  Droo kwa ajili ya kupanga mechi za hatua ya robo fainali inatarajiwa kufanyika jumatatu ijayo Septemba 3 katika makao makuu ya CAF mjini Cairo, na mechi hizo zitachezwa Septemba 14-16 kwa mechi za raundi ya kwanza, na raundi ya marudiano itakuwa kati Septemba 21-23.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako