• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yaagiza simu za mkononi zenye thamani ya Shs125bn katika nusu ya kwanza ya mwaka 2018

    (GMT+08:00) 2018-08-29 19:59:59

    Chapa ya simu ya Tecno iliagiza simu nyingi zaidi kuliko chapa nyingine zozote nchini Uganda katika nusu ya kwanza ya mwaka 2018,na kuzipiku chapa za Samsung,Nokia,na Apple ambazo zilitawala soko miaka iliyopita.

    Kulingana na takwimu kutoka Mamlaka ya Mapato Uganda (URA),kampuni hiyo ya simu kutoka China,iliingiza nchini humo simu za mkononi milioni 22 ikifuatiwa na Itel iliyoagiza simu za mkononi milioni 12.5 ikifuatiwa na Nokia.

    Samsung ilishika nafasi ya nne ikiwa na simu milioni 7.2 huku Apple ikiwa ya sita kwa kuagiza simu za mkononi 707,567.

    Infinix, Alcatel, Admet, Huawei na HTC zinajumuisha orodha ya chapa 10 za simu zilizoagizwa zaidi nchini Uganda katika nusu ya kwanza ya mwaka 2018 ulioisha tarehe 30 Juni.

    China ndio chanzo kikuu cha uagizaji wa simu katika kipindi hicho,ambapo simu zilizoletwa zilikuwa za thamani ya USh113.5b.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako