• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Serikali yaahidi kuimarisha sekta binafsi

    (GMT+08:00) 2018-08-29 20:00:28

    Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ameihakikishia sekta binafsi nchini humo kuwa serikali itaendelea kuweka mazingira bora yatakayoisaidia sekta binafsi kukua kwa kasi inayostahili.

    Akifungua mkutano wa 18 wa taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) jijini Dar es Salaam jana,Majaliwa alisema serikali itaendelea kufanya maboresho ya sera na sheria mbalimbali za usimamizi wa biashara ili kutoa nafasi ya ukuaji wa sekta binafsi na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

    Aidha alipongeza kaulimbiu ya mkutano wa mwaka ya uongozi wa biashara unaowajibika katika ushirikiano wa sekta za umma na binafsi kwa maendeleo endelevu ya uchumi.

    Majaliwa ambaye alimwakilisha Rais Magufuli katika mkutano huo,alisema serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara ikiwamo

    kuweka vivutio mbalimbali vitakavyosaidia ukuaji na maendeleo ya sekta binafsi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako