• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda-Sekta ya Utalii yaingiza $438m mwaka 2017

    (GMT+08:00) 2018-08-29 20:01:54

    Sekta ya utalii nchini Rwanda imeingiza mapato ya $438M mwaka 2017 kutoka $404M mwaka 2016.

    Haya ni kwa mujibu wa Ripoti ya mwaka ya Bodi ya Maendeleo ya Rwanda.

    Hata hivyo sekta hiyo haikufikia malengo yake ya $440M.

    Mapato hayo yalichangiwa mno na wasafiri wa kibiashara ambao waliingiza asilimia 33 ya mapato hayo huku asilimia 29 ikiandikishwa na wanaozuru nchi.Watalii nao walichangia asilimia 29 ya mapato hayo.

    Rwanda iliandikisha wajumbe 28,308 mwaka 2017, kutoka wajumbe 23,804 mwaka 2016 huku mikutano,makongamano na maonyesho yakichangia $42 milioni mwaka 2017 (kutoka $47M mwaka 2016).

    Sekta hiyo ndogo inatarajiwa kuongeza mchango wake wa mapato hadi $74M mwaka 2018.

    Nchi hiyo inakadiriwa imekuwa mwenyeji wa mikutano 169 ya kimataifa huku thuluthi ya mikutano hiyo ikiandaliwa na kitengo kipya cha Mikutano cha Rwanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako