• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Wakulima wa pamba eneo la Mpeketoni,Lamu,wapata hasara baada ya mashamba kuvamiwa na wadudu

    (GMT+08:00) 2018-08-29 20:02:15

    Wakulima wa zao la pamba katika tarafa ya Mpeketoni,kaunti ya Lamu wanakadiria hasara ya mamilioni ya pesa kufuatia uvamizi wa wadudu aina ya Red Sniper katika mashamba yao.

    Wakulima hao wapatao 10,000 wanasema kwamba zaidi ya ekari 10,000 za pamba zimeharibiwa na wadudu aina ya Red Sniper Mite.

    Msemaji wa wakulima wa pamba kaunti ya Lamu,Joseph Migwi amesema wakulima wanahofia mwaka huu hawatavuna chochote ,na kukosekana kwa zao hilo mwaka huu huenda kukasababisha wanafunzi kufukuzwa shuleni kutokana na ukosefu wa karo.

    Wakulima wengi wa pamba katika eneo la mpeketoni hutegemea kilimo cha zao hilo katika kujikimu kimaisha.

    Wakulima hao wametoa wito kwa serikali ya kaunti ya Lamu na ile ya Kitaifa kuwasaidia kukabiliana na wadudu hao waharibifu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako