• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Cote d'Ivoire wafanya mazungumzo

    (GMT+08:00) 2018-08-30 16:25:17

    Rais Xi Jinping wa China amekutana na rais Alassane Ouattara wa Cote d'Ivoire leo hapa Beijing, ambapo wamekubaliana kusukuma mbele uhusiano kati ya pande hizo mbili hadi kwenye kiwango cha juu zaidi, kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja.

    Leo asubuhi Rais Xi Jinping ameandaa sherehe ya kumkaribisha rais Alassane Ouattara wa Cote d'Ivoire ambaye ni kiongozi wa kwanza wa nchi za Afrika kufanya ziara ya kitaifa nchini China wakati wa mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC kwenye Jumba la mikutano la umma hapa Beijing. Kwenye mazungumzo kati ya viongozi hao wawili, rais Xi anasema:

    "Tunafurahi kukupokea rais Ouattara ukiwa ni kiongozi wa kwanza wa nchi za Afrika kuefanya ziara ya kitaifa wakati wa mkutano wa kilele wa FOCAC. Naamini kuwa mazungumzo kati yetu yatapata mafanikio na kuweka mwanzo mzuri wa ziara yako ya kitaifa nchini China na mkutano wa kilele wa FOCAC utakaofanyika hivi karibuni."

    Huu ni mwaka wa 35 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Cote d'Ivoire. rais Xi ameeleza kuwa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali umekuwa ukipanuka na kupata mafanikio. Siku hiyo chini ya usimamizi wa viongozi hao wawili, idara husika za pande hizo mbili zilisaini nyaraka za ushirikiano. Rais Ouattara anasema:

    "Pendekezo lako la 'Ukanda mmoja,Njia moja' lina umuhimu mkubwa na tunaliunga mkono kwa dhati. Pia nafurahi kwa kuweza kusaini nyaraka za ushirikiano kuhusu pendekezo hilo safari hii."

    Mkutano wa kilele wa FOCAC wa mwaka 2018 utawakutanisha viongozi wa nchi mbalimbali za Afrika, mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, pamoja na mashirika 27 ya kimataifa na Afrika utafanyika hivi karibuni. Kwenye mazungumzo na rais Ouattara, rais Xi anasema:

    "Mkutano huo unalenga kujenga jumuiya kati ya China na Afrika yenye hatma ya pamoja, na kukuza ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya pande hizo mbili, ambao pia una umuhimu mkubwa katika kuimarisha mshikamano kati ya nchi zinazoendelea duniani."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako