• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Wabunge wapanga kupunguza adhabu ya kuchelewa kulipa kodi kutoka 20% hadi 5%.

    (GMT+08:00) 2018-08-30 20:11:24

    Watu binafsi na makampuni ambayo yanashindwa kulipa kodi kwa wakati ufaao huenda wakapata afueni iwapo wabunge watapitisha mapendekezo ya kupunguza adhabu ya kuchelewa kulipa kodi kutoka asilimia 20 hadi asilimia 5.

    Kamati ya Fedha na Mipango ya Kitaifa inataka kurekebisha Sheria ya Kodi ya mwaka 2015,ili kupunguza adhabu wanazopewa walipa ushuru ambao wanachelewa kufanya marejesho ya kodi na kupitisha makataa ya tarehe 30 juni.

    Kamati hiyo aidha inapendekeza marekebisho mengine katika Mswada wa Fedha wa 2018 ambao utawasilishwa kwa ajili ya ukaguzi na upitishwaji wa mwisho wiki hii.

    Kamati hiyo inayoongozwa na Joseph Limo inasema marekebisho wanayotaka yafanywe katika mswada huo ni katika ibara ya 83A kwa kufuta neon 20 na kulibadilisha na neno 5.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako