• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Bandari ya Mtwara kupokea lita milioni 9.6 za mafuta

    (GMT+08:00) 2018-08-30 20:11:53

    Bandari ya Mtwara inatarajia kupokea lita milioni 9.6 za mafuta (tani ujazo 8,000) mwezi ujao,ikiwa ni mara ya pili kwa bandari hiyo kupokea shehena tangu Juni,mwaka huu.

    Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Uagizaji mafuta pamoja kwa Pamoja (PBPA),Erasto Simon,alisema hayo jana mjini Mtwara alipokuwa akiwasilisha ripoti ya Wizara ya Nishati kuhusu uanzishwaji wa gati la kupokelea mafuta katika bandari ya Mtwara mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

    Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu na Katibu Mkuu wa Wizara,Dk Hamisi Mwinyimvua,waliwaongoza watendaji mbalimbali wa wizara na taasisi zake katika utoaji wa taarifa na ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwenye kamati hiyo.

    Erasto Simon alisema tani za ujazo 8,000 zinatarajiwa kushushwa katika bandari ya Mtwara ifikapo Septemba 5 na tani 5,000 kati ya hizo zitakuwa mafuta ya dizeli na tani 3,000 zitakuwa petrol.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako