• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa Afrika Kusini nchini China aeleza ushirikiano kati ya nchi mbili

    (GMT+08:00) 2018-08-31 09:21:15

    "Katika makumi ya miaka iliyopita, China na Afrika zimeshirikiana na kushikamana kwa dhati. Zinadumisha hali ya kuwa jumuiya yenye hatma na maslahi ya pamoja." hayo yamesemwa na rais Xi Jinping wa China wakati alipotembelea Afrika mwezi Juni, mwaka huu. Mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika. FOCAC utakaofanyika hivi karibuni, unafuatiliwa sana duniani. Kabla ya kufunguliwa kwa mkutano huo, waandishi wa habari wa CRI wamefanya mahojiano na mabalozi wa Tanzania, Zimbabwe, Rwanda, Uganda, Burundi na Afrika Kusini nchini China, kuhusu mafanikio na maendeleo yaliyopatikana chini ya mfumo wa FOCAC, kuhimiza ujenzi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja ili kupata maslahi ya pamoja ya China na Afrika. Hivi karibuni tumemhoji balozi wa Afrika Kusini nchini China Bibi Dolana Msimang akieleza ushirikiano kati ya China na Afrika Kusini.

    Mwanahabari: Kuna fursa nyingi za ushirikiano kati ya China na Afrika Kusini, unaweza kutueleza maendeleo ya hivi karibuni katika kuimarisha ushirikiano wa pande mbili kati ya nchi hizi mbili?

    Baozi: Kwanza ningependa kusema kwamba mwaka huu tunaadhimisha miaka 20 ya kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Afrika Kusini. Kabla ya hapo kulikuwa na uhusiano kwa sababu China iliunga mkono Afrika Kusini katika kupambana na ubaguzi wa rangi lakini pia tuna ushahidi wa biashara kati yetu na China kati ya 12 00 AD na 13 00 AD. Baada ya kuanzisha uhusiano wetu miaka 20 iliyopita tulipanda ngazi na kuwa na ushirikiano wa kimkakati na kisha kuongeza zaidi na kuwa na ushirikiano wa mkakati wa kina. Uhusiano wetu unafuata msingi wa uaminifu kati ya pande zote mbili na pia kujaribu kuwa na matokeo ya pamoja. Hivi sasa China ndio mshirika wetu mkubwa wa biashara na imekuwa mshirika wetu mkuu wa biashara kwa miaka tisa iliyopita. Tulipoanzisha mahusiano yetu ya kidiplomasia, China haikuwa imeorodheshwa kwenye washirika 10 bora wakibiashara na Afrika Kusini lakini sasa imekuwa sio tu mshirika mkuu lakini pia kwa miaka tisa. Biashara yetu imeongezeka kutoka rand bilioni 1.8 tu mwaka 1994 hadi rand bilioni 318 mwaka 2017, na sasa tumeongeza mwelekeo mwingine kwa uhusiano wetu mwaka jana. Aliyekuwa Makamu wa rais wa China Liu Yandong alikwenda Afrika Kusini ili kuanza kuzindua kikao cha kwanza cha kuanzisha uhusiano wa mabadilishano ya wa watu kwa watu. Kwa hiyo hilo linatutia nguvu badala ya kubadilishana tu kwenye sekta za kiuchumi na kisiasa, pia tunabadilishana kwenye Nyanja za afya, sayansi, elimu na teknolojia. Lakini pia kuna nafasi nyingi za kuboresha. Kutokana na ukubwa na uwezo wa China na pia uwezo wa Afrika Kusini, nadhani huu ni mwanzoo tu na bado kuna mengi zaidi ya kufanya.

    Mwanahabari: Nchi kumi zinazoibuka kwa kasi duniani ni pamoja na nchi zuta kutoka Afrika. Ushirikiano wa China na Afrika una nafasi gani katika kuboresha

    Balozi: Ningependa kusema kuwa China inatekeleza jukumu muhimu na kama ulivyosema jukumu lao linaendana vizuri na Afrika kwa sababu bara hilo ndio litakua kitovu kijacho cha ukuaji dunaini. Umeeleza kuwa Afrika ina nchi sita kati ya kumi zinazokua kwa haraka kiuchumi na hiyo kati yetu kumi inaonyesha kwamba kwanza idadi yetu ya watu inakua na pili uchumi wetu unakua na tuna kiwango cha ukuaji wa juu, tuna idadi kubwa zaidi ya vijana na hivyo Afrika ina uwezo mkubwa. Afrika iko nyuma ikilinganishwa na mabara mengine na ili kubadili hilo utahitaji kuweka mipango mingi ya maendeleo. China has single handedly taken on things that are sometimes handled by organizations which consists many countries and have done well in the process. China imetekeleza jukumu muhimu katika kufanya hivyo. Wakati wa mkutano wa mwisho wa FOCAC huko Johannesburg Rais Xi Jinping aliahidi dola bilioni 60 za Marekani na lengo lake lilikuwa ni kujaribu kuendeleza uchumi wa Afrika na fedha hizo zilisaidia katika maendeleo ya miundombinu, katika maendeleo ya ujuzi, kilimo cha kisasa na pia kuboresha uchumi wa baharini. Kuna mengi ambayo yamefanikishwa lakini kuna pengo kubwa ambalo linapaswa kuzibwa na China imekuwa kwenye msitari wa mbele kuleta mabadiliko. China ikiwa nchi moja imekuwa ikitekeleza miradi ambayo mara nyingi hutekelezwa na mashirika ya kimataifa na imefanya vizuri katika hilo.

    Mwanahabari: China imekuwa na ushawishi mkubwa wa kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja, lakini kuna sauti za pingamizi zinazotokea nchi za magharibi, pia tunasikia "vitendo vya upande mmoja" kutoka kwenye nyanja za kisiasa. Kuna hatari zozote kwenye maslahi yetu ya pamoja kwa sasa?

    Balozi: Nadhani tumeendeleza uhusiano wetu na kufikia kiwango ambapo hatupaswi kuharibiwa au kuathriwa na mambo kama hayo na nadhani tukizingatia suala hilo la heshima kwa pande mbili na faida ya pamoja kati yetu hakuna chochote kinachoweza kuvunja uhusiano huo. Bila shaka Afrika inapaswa kulinda maslahi yake yenyewe, China haiwezi kufanya mambo kwa ajili ya Afrika, lakini China itashirikiana na Afrika ili kufanya baadhi mambo Mwisho wa siku Afrika lazima iweze kufanikisha upande wake ili uhusiano ustawi. Lakini uhusiano wetu umepitia nyakati ngumu na umeendelea kuongezeka haujaanguka. Baadhi ya maoni yanayotokea yanatoka kwa watu ambao tulikuwa na uhusiano mzuri nao awali na sasa wanahisi uchungu wa kugawana nafasi na China hivyo mara nyingi ni shinikizo la kuwa na kushiriki nafasi ambayo ilikuwa ya kipekee tu kwa nchi za magharibi. Na China sasa inatoa fursa yenye faida ambayo haikuwa inapatikana awali. China na Afrika Kusini zina uhusiano imara sana. Ninaweza kuthibitisha hilo kwa sababu ni nchi yangu, Rais Xi Jinping amekamilisha ziara yake nchini Afrika Kusini na Rais wetu atakuja hapa hivi karibuni. Tuna msingi imara sana ambao haujabadilishwa hata na serikali tofauti zinazoendesha nchi. Imefikia kiwango ambapo kila kitu kinaenda vizuri. Bara la Afrika lina uhusiano wa muda mrefu na kile ambacho China ilifanya ni kwamba pia iliunganisha maslahi yake pamoja na malengo ya maendeleo ya Afrika na kuchukua mwelekeo wa pale Afrika ingependa kuwa mwaka wa 2063. Kwa hiyo inawezesha China kushirikiana nasi vizuri. Haikuja na mipango yake mwenyewe lakini ilijiunga kwenye mipango ambayo iko ndani ya Afrika. Kile kinachoweza kuwavutia zaidi wachina ni kwamba Afrika Kusini ina idadi kubwa ya watu wa China na tuna idadi ya watu kadhaa wenye asili ya Kichina ambao sasa wamepata uraia wa Afrika Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako