• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa sita wa wafanyabiashara wa China na Afrika kufanyika hapa Beijing

    (GMT+08:00) 2018-08-31 19:11:57

    Mkutano wa sita wa wafanyabiashara wa China na Afrika utafanyika kando ya Mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao.

    Wajumbe karibu elfu moja wa sekta ya viwanda na biashara kutoka nchi 53 za Afrika na wadau wa China watajadili ushirikiano wa sekta za utandawazi wa viwanda, biashara, na ujenzi wa miundo mbinu ili kusaidia ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika na ukuaji wa uchumi wa dunia.

    Mkutano huo wa siku mbili unaoandaliwa na kamati ya kuhimiza biashara za kimataifa ya China na wizara ya biashara ya China. Shughuli mbalimbali pia zitafanyika ikiwemo mazungumzo ya wakurugenzi wakuu wa China na Afrika, baraza la maendeleo ya mtandao wa Internet wa nishati wa Afrika, mkutano wa kutangaza miradi ya wenzi wa ushirikiano wa uwekezaji na ukuaji wa Afrika, na mazungumzo ya mawasiliano ya kampuni za China na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako