• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na marais wa Sudan Kusini na Niger

    (GMT+08:00) 2018-08-31 20:12:29

    Rais Xi Jinping wa China hapa Beijing amekutana kwa nyakati tofauti na rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na rais Mahamadou Issoufou wa Niger.

    Katika mazungumzo yake na rais Kiir, rais Xi amezipongeza pande mbalimbali za Sudan Kusini kwa kusaini makubaliano ya amani ya pande zote. Amesema China itaendelea kuunga mkono mchakato wa amani wa nchi hiyo, kulinda maslahi ya nchi hiyo katika Umoja wa Mataifa na kutoa uungaji mkono kwa upatanishaji wa suala la Sudan Kusini wa mashirika ya kanda ya Afrika.

    Rais Kiir amesema, Sudan Kusini imepongeza China kwa kuwa na msimamo sawa kwenye mambo ya kimataifa kwa nchi kubwa au ndogo na kuunga mkono nchi mbalimbali kujichagulia njia ya kujiendeleza inayofaa hali halisi.

    Rais Xi alipokutana na rais Issoufou amesema, China inapendea kupanua ushirikiano na Niger katika sekta za matibabu, ujenzi wa miundombinu, nishati na usafiri, na kuunga mkono juhudi za nchi za Afrika Magharibi kuimarisha mawasiliano. Rais Issoufou amesema, Niger inapenda kuzidisha ushirikiano wenye ufanisi na China katika sekta mbalimbali ikiwemo uchumi na biashara, nishati na usalama.

    Baada ya mkutano huo, marais wa nchi hizo mbili pia wameshuhudia kusainiwa kwa nyaraka za ushirikiano wa pande mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako