• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya na Uingereza kushirikiana kiuchumi

    (GMT+08:00) 2018-08-31 20:39:57

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May wamefanya mkutano unaolenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya pande zote mbili. Kwenye hotuba ya viongozi hao uwekezaji na sekta ya biashara zilionekana kuegemewa pakubwa.

    Kenyatta ameeleza kwamba wameafikiana na May kuimarisha sekta ya biashara kati ya Kenya na Uingereza, hasa chini ya Jumuiya ya Madola ambapo mataifa yote mawili ni wanachama. Uhuru ameongeza kuwa mataifa yote mawili kuwa wanachama wa Jumuiya ya Madola, itasaidia kupiga jeki sekta ya biashara ambapo nafasi za ajira zitafunguka.

    Nguzo za ajenda kuu nne ambazo ni; kuimarisha sekta ya afya kwa matibabu bora kwa kila Mkenya, ujenzi wa viwanda na kampuni kutatua ukosefu wa ajira hususan kwa vijana, makazi nafuu na bora, na kuangazia usalama wa chakula, pia zimejadiliwa na viongozi hao. Kwa upande wake, Waziri May amesema Uingereza imejitolea kwa hali na mali kuhakikisha uhusiano kati ya Kenya na Uingereza umeimarika na kusisitiza kuwa Uingereza ni mmoja wa mwekezaji mkuu nchini Kenya. Wakati huo huo viongozi hao wawili wamesaini mkataba wa kurejesha mabilioni ya pesa yaliyotoroshewa Uingereza kinyume cha sheria. Kabla ya May kuwasili Kenya, rais Kenyatta alikuwa Marekani akifanya mazungumzo na Rais Donald Trump na kusaini makubaliano kadha ya kibiashara yenye thamani ya Dola 900 milioni. May ataelekea China kwenda kushiriki mkutano wa uhusiano baina ya China na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako