• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TRA yatangaza msamaha kwa walipakodi

    (GMT+08:00) 2018-08-31 20:41:33

    Kamishna wa TRA Bw.Charles Kichere ametangaza msamaha kwa walipakodi wenye malimbikizo ya madeni ya riba na adhabu na kuwapa fursa ya kulipa kodi ya msingi mara moja au kwa awamu. TRA imetangaza msamaha wa riba na adhabu kwenye malimbikizo ya madeni ya kodi kwa asilimia 100 tofauti na asilimia 50 ilivyokuwa hapo awali.

    Msamaha huo umetokana na malalamiko ya wafanyabiashara waliyoyatoa kwa rais John Magufuli kuhusu malimbikizo makubwa ya madeni ya kodi za nyuma ikiwemo riba na adhabu yanayowakabili. Walitoa malalamiko hayo kwenye mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) uliofanyika Machi. Rais aliwaambia wafanyabiashara hao wazungumze na Wizara ya Fedha na Mipango kupata suluhu la kudumu.

    Baada ya mkutano huo, Bunge la Bajeti lilipitisha marekebisho ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi na kumpa mamlaka waziri mwenye dhamana kutoa msamaha wa riba na adhabu kwenye malimbikizo ya madeni ya kodi ya nyuma.

    Baada ya marekebisho hayo, waziri amemuagiza kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutoa msamaha maalumu wa riba na adhabu kwenye malimbikizo ya madeni ya kodi kwa asilimia 100.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako