• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyabiashara wa soko la Jubilee Kenya waanza kubomoa vibanda vyao

    (GMT+08:00) 2018-08-31 20:41:48

    Wafanyibiashara wa soko la Jubilee mtaani Githurai 45, Kiambu wameanza kubomoa vibanda vyao. Hatua hiyo imejiri wiki moja baada ya Gavana Ferdinand Waititu kufanya mkutano nao na kuwaeleza kuwa halmashauri ya kitaifa ya barabara kuu nchini (KenHa) inalenga kuunda egesho la magari katika ardhi iliyotumika na wafanyabiashara hao.

    Waititu pia aliwaambia sehemu nyingine ya ardhi hiyo itajengwa soko la kisasa, akifafanua kwamba litakuwa la ghorofa nne. Walikuwa wamepewa makataa ya wiki moja kufanya ubomozi wa vibanda vyao.

    Wafanyabiashara na wachuuzi hao, wameamua kubomoa vibanda vyao kwa hiari. Hata hivyo, baadhi yao wameeleza shauku kuhusu ujenzi wa soko hilo.

    Ijumaa wiki jana, baada ya Gavana Waititu kufanya kikao nao, alichapisha ujumbe kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba wafanyabiashara wa Jubilee Market wamekubali kujengewa soko la kisasa katika ardhi waliyokuwa.

    Akihutubia wafanyabiashara hao alisema ujenzi wa soko hilo unaofadhiliwa na serikali ya kitaifa utagharimu zaidi ya Sh2 bilioni. Alisema kuwa ujenzi wa soko hilo ni kufuatia ahadi ya Rais Uhuru Kenyatta ya awali kwa wafanyabiashara hao kuwajengea soko la kisasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako