• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Standard Chartered kuipatia Tanzania mkopo nafuu

    (GMT+08:00) 2018-08-31 20:42:06

    Benki ya Standard Chartered Group imekubali kuipatia Tanzania mkopo nafuu wa Dola za Marekani bilioni 1.46 kwa ajili ya kujenga kipande cha Reli ya Kiwango cha Kimataifa (SGR) kuanzia Morogoro hadi Makutupora, mkoani Dodoma.

    Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Dk. Philip Mpango, ameyasema hayo alipokutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bill Winters, jijini Dar es Salaam.

    Dk. Mpango alimweleza Bw Winters anayeongoza benki hiyo kwenye nchi zaidi ya 60 duniani, kuhusu vipaumbele vikubwa vya nchi ikiwemo kuboresha Kampuni ya Ndege Tanzania(ATCL) na ujenzi wa mradi wa kufufua umeme wa Mto Rufiji.

    Amesema Tanzania ni ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii ikitanguliwa na Brazil, lakini inapokea watalii wasiozidi milioni mbili kwa mwaka jambo ambalo linahitaji kufanyiwa kazi kwa haraka ili sekta hiyo ichangie uchumi wa nchi kwa kiasi kikubwa kupitia fedha za kigeni.

    Winters ameipongeza Tanzania kwa kupiga hatua kubwa kiuchumi na kusema kwamba benki yake itatoa mkopo huo na kuahidi kuwa balozi wa kuelezea mafanikio makubwa ya kiuchumi ya Tanzania kwa wadau wengine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako