• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msemaji wa serikali ya Tanzania: "uzoefu wa China" utasaidia ukuaji wa uchumi wa Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-09-01 16:26:08

    Msemaji wa serikali ya Tanzania Bw. Hassan Abbas amesema Tanzania inafaa kuiga "uzoefu wa China", na pendekezo lililotolewa na China la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" litasaidia ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo.

    Akizungumza na mwandishi wetu wa habari, Bw. Abbas amesema, kutokana na uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, China imepata mafanikio makubwa. Ili kubadilisha sura ya kuwa nyuma kimaendeleo, China imezindua njia ya siasa ya ujamaa wenye umaalum wa kichina. Tanzania na China zimeshuhudia historia inayofanana ya maendeleo na zinakabiliwa na changamoto zinazofanana katika maendeleo ya uchumi, hivyo Tanzania inastahili kujifunza "uzoefu wa China" ili kusaidia maendeleo ya uchumi wake.

    "Kutokana na uongozi imara wa Chama cha Kikomunisti cha China, China imepata mafanikio makubwa. Serikali ya China imejitafutia njia ya maendeleo inayolingana na sifa yake maalumu na kuitekeleza. Kama tunavyoshuhudia leo, kila mji wa China umejaa uchangamfu na uhai. Tunastahili kujifunza uzoefu wa China."

    Bw. Abbas pia amesema, mbali na kujiendeleza, China pia imesaidia nchi nyingine kutafuta maendeleo. Mpango wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" uliotolewa mwaka 2013 umenufaisha nchi nyingi. Ametoa mfano wa Tanzania, na kwamba kumekuwa na kampuni nyingi za China zimewekeza na kujenga viwanda kuhusiana na nyanja mbalimbali za Tanzania. Kampuni kubwa zaidi ya kutengeneza vioo katika kanda ya Afrika Mashariki, kampuni ya vioo na viwanda ya Afrika iliyoko katika eneo la Mkuranga ndio tunda la ushirikiano wa mradi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kati ya nchi hizo mbili. Hivi karibuni, maandalizi ya ujenzi wa reli ya kisasa itakayojengwa kwa pamoja na serikali za China na Tanzania pia yalianza. Bw. Abbas amesema hivi sasa, Tanzania imefungua mlango wa viwanda na uwekezaji kwa dunia, na inaaminika kuwa "uzoefu wa China" utasaidia ukuaji wa uchumi wa Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako