• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa asema ushirikiano kati ya China na Afrika ni muhimu kwa amani na maendeleo ya Afrika na dunia

    (GMT+08:00) 2018-09-01 18:48:19

    Kabla ya kuhudhuria mkutano wa kilele wa FOCAC mjini Beijing kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres, alihojiwa na waandishi wa habari wa China na kusema kuwa ushirikiano kati ya China na Afrika unatoa fursa muhimu kwa maendeleo ya China na kuhimiza nchi za Afrika kupata maendeleo katika sekta za uwekeaji wa uchumi na biashara, utulivu wa jamii na maendeleo endelevu.

    "mkutano viongozi wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika utakaofanyika hivi karibuni mjini Beijing ni muhimu sana, viongozi wa China na nchi za Afrika watafanya majadiliano kuhusu masuala ya ushirikiano yanayofuatiliwa na pande hizo mbili. Ushirikiano kati yao ni muhimu kwa mafanikio ya Afrika, na pia mafanikio ya Afrika ni muhimu kwa amani na maendeleo ya dunia."

    Bw. Guterres amesema kuwa, atahudhuria mkutano huo nchini China kwa ajili ya kuonyesha uungaji mkono wa Umoja wa Mataifa kwa ushirikiano kati ya China na Afrika na ufuatiliaji kwa ushirikiano wa Kusini na Kusini.

    "Ushirikiano kati ya China na Afrika ni sehemu ya kiini ya ushirikiano wa Kusini na Kusini. Ushirikiano wa Kusini na Kusini unaongezeka kuwa wa muhimu siku hadi siku. Lakini ushirikiano wa Kusini na Kusini hauwezi kuwa mbadala wa ushirikiano wa Kusini na Kaskazini. Nchi zilizoendelea zinapaswa kutekeleza majukumu yao kwa nchi zinazoendelea katika ushirikiano wa kimataifa. Tumeona kuwa, katika miongo kadhaa iliyopita, China imenufaisha ushirikiano kati yake na nchi za Afrika kwa mafanikio yake yaliyopatikana katika maendeleo ya uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako