• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa 7 wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika wafanyika hapa Beijing

    (GMT+08:00) 2018-09-02 18:19:02

    Mkutano wa 7 wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika umefanyika leo hapa Beijing. Mjumbe wa taifa wa China ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi na waziri wa biashara wa China Bw. Zhong Shan waliendesha mkutano huo pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusini Bi. Lindiwe Sisulu na waziri wa biashara na viwanda wa Afrika Kusini Bw. Robert Haydn Davies. Mawaziri wa mambo ya nje na mawaziri na wajumbe wa biashara ya nje, kutoka nchi 53 wanchama wa wa Afrika pamoja na wajumbe wa kamati ya Umoja wa Afrika wamehudhuria mkutano huo.

    Bw. Wang Yi na Bw. Zhong Shan walitoa ripoti katika mkutano huo kuhusu hali ya utekelezaji baada ya mkutano wa kilele wa Johanesburg wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika.

    Bw. Wang Yi pia amesema kuwa mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika utafanyika kesho, kiwango cha mkutano huo kitafikia ngazi ya juu zaidi, ambapo rais Xi Jinping wa China na rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kuisni wataendesha kwa pamoja mkutano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako