• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China akutana na rais wa Sudan

    (GMT+08:00) 2018-09-03 07:52:39

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amekutana na rais Omar al-Bashir wa Sudan Kusini hapa Beijing., na kumwambia China inathamini urafiki wa jadi kati yake na Sudan, na siku zote inaichukulia Sudan kama ni rafiki na mwenzi mzuri barani Afrika na katika nchi za kiarabu.

    Amesema China inaunga mkono Sudan kujiamulia njia za kujiendeleza na juhudi za kulinda amani, na inapenda kushirikiana zaidi na Sudan, kuimarisha ushirikiano katika kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja, Njia Moja", kupanua ushirikiano katika biashara, uwekezaji na kilimo, na kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii kati ya nchi hizo mbili.

    Rais Bashir amesema mwaka kesho utakuwa ni wa miaka 60 tangu Sudan na China zianzishe uhusiano wa kibalozi, na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili umepata mafanikio katika sekta mbalimbali na utakuwa na mustakbali mzuri. Ameishukuru China kwa kutoa msaada kulinda utulivu na maendeleo ya Sudan, na ushirikiano kati ya Sudan na China umehimiza zaidi ushirikiano kati ya Kusini na Kusini na kati ya Afrika na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako