• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Maurius zamaliza mazungumzo kuhusu makubaliano ya biashara huria

    (GMT+08:00) 2018-09-03 13:40:18

    China na Mauritius zimemaliza mazungumzo kuhusu makubaliano ya biashara huria kati yao, ambayo yatakuwa ni ya kwanza ya aina hiyo kutarajiwa kusainiwa kati ya China na nchi ya Afrika, na nchi hizo mbili zitafanya maandalizi kwa ajili ya kusainiwa kwake rasmi.

    Jana naibu waziri wa biashara wa China Gao Yan na waziri wa mambo ya nje, ushirikiano wa kikanda na biashara ya kimataifa wa Mauritius Seetanah Lutchmeenaraidoo walisaini kumbukumbu ya maelewano ya Wizara ya Biashara ya China na Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Biashara Huria kuhusu kumaliza mazungumzo ya makubaliano ya biashara huria kati ya nchi zhizo mbili.

    Mazungumzo hayo yalianza rasmi mwezi Disemba mwaja jana, na yametimiza malengo ya "pande zote, kiwango cha juu, na kunufaishana", na yamehusisha sekta mbalimbali nyingi zikiwemo biashara ya mizigo, biashara ya huduma, uwekezaji, na ushirikiano wa kiuchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako