• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China inaunga mkono nchi za Afrika kushiriki kwenye ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kunufaika kwa pamoja na matunda yake

    (GMT+08:00) 2018-09-03 15:19:16

    Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amehudhuria mkutano wa ngazi ya juu wa viongozi na wadau wa viwanda na biashara kati ya China na Afrika na ufunguzi wa mkutano wa 6 wa wajasiriamali kati ya China na Afrika. Katika hotuba yake yenye kichwa cha "kuelekea kwa pamoja njia ya kujitajirisha", rais Xi amesisitiza kuwa China inaunga mkono nchi za Afrika kushiriki kwenye ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", kupenda kufanya kazi na Afrika katika kuunganisha mikakati yao, na kujenga njia ya kujiendeleza ya kiwango cha juu inayoendana na hali halisi ya nchi, inayowashirikisha na kuwanufaisha watu wote, kusaidiana na kunufaishana, ili kuboresha maisha ya watu.

    Rais Xi amesema mipango 10 ya ushirikiano aliyotangaza kwenye mkutano wa kilele wa Johannesburg wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika miaka mitatu iliyopita, imepata matunda mengi. China na nchi za Afrika zimezidi kuunganisha mikakati yao, kuimarisha mawasiliano ya kiuchumi na kibiashara, na kupata maendeleo makubwa katika mchakato wa maendeleo ya kiviwanda na mambo ya kisasa, ujenzi wa miundombinu, urahisi wa biashara na uwekezaji, ujenzi wa uwezo, na kupunguza umaskini, na mafanikio hayo ya ushirikiano kati ya China na Afrika yanawanufaisha watu wa Afrika.

    Rais Xi amesisitiza kuwa watu wa Afrika wanachukua moja kati ya sita ya watu wote duniani, na kutimiza utajiri wa pamoja wa watu wote duniani wakiwemo watu wa Afrika ni sehemu muhimu ya kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja. China na Afrika ni marafiki wa muda mrefu, na zilikuwa ndugu wazuri waliopambana na maadui kutoka nje bega kwa bega na sasa ni wenzi wazuri wanaotafuta maendeleo kwa pamoja. China na Afrika zimekuwa jumuiya yenye hatma ya pamoja inayofurahia ustawi na kukabiliana na changamoto kwa pamoja, pia ni jumuiya yenye maslahi ya pamoja inayofanya ushirikiano wa kunufaishana. China na Afrika ziko mbele katika mchakato wa historia wa kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

    Rais Xi amesema Afrika ni washiriki muhimu katika kujenga "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kwa mujibu wa historia na jiografia, na China inaunga mkono nchi za Afrika kushiriki kwenye ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Katika msingi wa usawa na kusaidiana, na kufuata kanuni za kushauriana, kujenga kwa pamoja na kunufaishana, China inapenda kufanya kazi pamoja na Afrika katika kuunganisha mikakati yao, kuhimiza uratibu kuhusu sera, kuunganishwa kwa vifaa, biashara rahisi, mafungamano ya kifedha na maelewano kati ya watu, na na kujenga njia ya kujiendeleza ya kiwango cha juu inayoendana na hali halisi ya nchi, inayowashirikisha na kuwanufaisha watu wote, kusaidiana na kunufaishana.

    Rais Xi amesema huu ni mwaka wa 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango. Bila ya kujali jinsi hali ya kimataifa inavyobadilika, China itaendelea kufungua mlango wake kwa nje bila ya kusita, na kwa uwazi zaidi. China inawakaribisha wajasiriamali wa nchi mbalimbali wakiwemo wale kutoka Afrika kuja China kufanya shughuli za biashara, na pia kuwahamasisha wajasiriamali wa China kwenda Afrika kutafuta fursa za kujiendeleza ili kushirikiana kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

    Rais ametoa matumaini manne kwa wajasiriamali wa China na Afrika: moja ni kuweka kipaumbele kwa maslahi ya China na Afrika, kuwa na upeo wa kuona mbali, na kufanya juhudi, na watu wa China na Afrika kukua kwa pamoja na kupata mafanikio ya pamoja; pili, kushika vizuri fursa ya kihistoria yenye uvumbuzi, kupeana uzoefu, kuvumbua njia za ushirikiano, kutumia vizuri maendeleo ya teknolojia ya kisasa, kuendeleza sekta zinazojitokeza hivi karibuni na zenye mustakabali mzuri, na kuhimiza kuinua sekta ya viwanda vya jadi na kukuza sekta ya akili bandia; tatu, kubeba majukumu ya kijamii, kuheshimu utamaduni na desturi za nchi wanazoishi na kufanya kazi, kuzingatia kuinua sifa ya kampuni, kutilia maanani kazi za kutoa mafunzo kwa wafanyakazi na kuboresha maisha ya wakazi wazawa, kutilia maanani uhifadhi wa mazingira na kubana matumizi ya maliasili ili kujenga mazingira mazuri kwa maendeleo ya muda mrefu. Nne, kujichukulia kama ni daraja la urafiki kati ya China na Afrika katika ushirikiano wa kiuchumi, kupanda mbegu ya urafiki katika mahali biashara wanapofanya na kujenga mnara wa urafiki mahali miradi inapojengwa.

    Viongozi 35 wa nchi za Afrika wanaoshiriki kwenye mkutano wa kilele wa Beijing wa FOCAC, wajasiriamali mashuhuri wa China na Afrika na wajumbe wa mashirika ya kimataifa wapatao elfu moja wamehudhuria ufunguzi wa mkutano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako