• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yatarajia mkutano wa FOCAC utahimiza kuunganisha pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja na ajenda ya mwaka 2063 ya Afrika

    (GMT+08:00) 2018-09-03 16:07:15
    Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Bw. Dirdiri Mohamed Ahmed amesema, anatarajia mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) unaoanza leo hapa Beijing utahimiza kuunganisha pendekezo la Ukanda moja na Njia moja na ajenda ya mwaka 2063 ya Afrika.
    Akizungumza hapa Beijing, Bw. Dirdiri amesema FOCAC ni jukwaa muhimu la kubadilishana uzoefu wa maendeleo kati ya nchi za Afrika na China, na pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" lililotolewa na China ni mpango muhimu wa kuwanufaisha watu wa nchi mbalimbali. Amesema Sudan itafanya juhudi kujiunga na ujenzi wa pendekezo hilo, na akitarajia mkutano huo utatoa mkakati mpya wa kuhimiza maendeleo ya nchi za Afrika na kuzidisha ushirikiano wa Kusini na Kusini.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako